LONDON.Gordon Brown adokeza kuwa yuko tayari kukiongoza chama cha Labour
25 Septemba 2006Matangazo
Waziri wa fedha wa Uingereza Gordon Brown na anaetarajiwa kuchukuwa mahala pa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema amefadhaishwa na migongano inayo endelea ndani ya chama kinachotawala cha Labour.
Akihutubia katika mkutano wa mwaka wa chama hicho bwana Brown alimsifu waziri mkuu Tony Blair ya kuwa ni kiongozi mwenye kuona mbali ijapokuwa kulikuwa na panda shuka katika uhusiano wao wa muda mrefu.
Waziri Brown pia amedokeza kuwa yupo tayari kukiongoza chama cha Labour.
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair bado hajatangaza rasmi ni lini atakapong’atuka madarakani hata ingawa alithibitisha kuwa hotuba yake ya leo ni ya mwisho kama kiongozi wa chama cha Labour.