LONDON: Waziri Mkuu Tony Blair atangaza mpango wa kung'atuka.
10 Mei 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, amelieleza baraza lake la mawaziri kuhusu mpango wake wa kung'atuka wadhifa wa kiongozi wa chama tawala cha Leba na pia uwaziri mkuu.
Tony Blair anatarajiwa baadaye kutangaza uamuzi wake huohadharani kwenye eneo lake la uwakilishi bungeni.
Waziri wa fedha Gordon Brown ndiye anayetarajiwa kumrithi Tony Blair.
Blair amesema ataendelea kuushikilia wadhifa wa kiongozi wa chama chake kwa kiasi miaka saba hadi pale kiongozi mpya atakapochaguliwa.