1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Watumishi wa Umoja wa Mataifa walaumiwa kwa ubakaji Sudan.

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdi

Watumishi wa Umoja wa Mataifa pamoja na askari wa kulinda amani katika eneo la kusini mwa Sudan wameshutumiwa kwa kuwabaka watoto, baadhi yao wakiwa na umri wa miaka kumi na miwili.

Gazeti la Daily Telgraph la Uingereza limearifu limekusanya taarifa kutoka kwa waathiriwa zaidi ya ishirini kutoka mji wa Juba.

Gazeti hilo limedai watoto hao walianza kubakwa tangu miaka miwili iliyopita, wakati Umoja wa Mataifa ulipoelekea kusini mwa Sudan kusaidia kukarabati eneo hilo lililokuwa limekabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaka ishirini na mitatu.

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani mjini New York, imekataa kuzungumzia suala hilo.