LONDON: Tony Blair waziri mkuu wa Uingereza na chama chake cha Labour washinda uchaguzi mkuu
6 Mei 2005Matangazo
Viongozi mbali mbali wa dunia wamempongeza waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na chake cha Labour kwa ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu wa hapo jana ambapo umemrudisha Waziri mkuu huyo kwa mara ya tatu mfululuzo katika kuingoza Uingereza.
Hata hivyo chama cha bwana Blair cha Labour kilishinda uchaguzi huo kwa wingi mdogo wa viti vya bunge 66.
Wakati huo huo Michael Howard kiongozi wa chama cha Conservative ametangaza atajiuzulu mara tu chama chake kitapompata mrithi wake.
Licha ya Kampeini za uchaguzi huo kumpa changamoto bwana Blair juu ya suala la vita vya Iraq mnamo mwaka 2003 ushindi wa Labour unafikiriwa umetokana na kampeini yake juu ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.