1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Tony Blair atangaza hatua mpya za kupambana na ugaidi.

6 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnV

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ametangaza hatua mpya kadha za kupambana na ugaidi baada ya kushambuliwa kwa mji wa London hivi karibuni.

Blair ametoa mapendekezo yapatayo kumi na mbili kuweza kupambana na viongozi wenye msimamo mkali wa dini ya Kiislamu ambao wanaunga mkono ugaidi ama kusambaza maneno ya chuki.

Moja kati ya hatua hizo za kutatanisha ni uwezekano wa kuangalia upya sheria ya haki za binadamu ya mwaka 1998, ambayo itaharakisha kurejeshwa kwa wageni ambao watahusishwa na ugaidi.

Mabadiliko mengine ni pamoja na kupigwa marufuku mara moja kwa makundi mawili ya Kiislamu yenye msimamo mkali. Kwa upande wake, mashirika yanayopigania haki za binadamu yameeleza wasi wasi wao kwa baadhi ya hatua hizo.