1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Tony Blair ataka mbinyo zaidi kwa Mugabe

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGa

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema atauchagiza Umoja wa Ulaya kuzidhisha mbinyo wa kivikwazo dhidi ya utawala wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Tony Blair aliliambia bunge la Uingereza kuwa ataliomba pia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa kauli kali dhidi ya hali nchi Zimbabwe aliyoiita ni ya kutisha.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza pia alitoa wito kwa viongozi wa nchi jirani na Zimbabwe, kusaidia kumshurutisha Mugabe kuwa na utawala Bora

Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai alikuwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho waliyojeruhiwa na polisi walipovunja maandamano yao.

Serikali ya Zimbabwe kwa upande wake imekuwa ikisema kuwa watu hao walikuwa wanavunja sheria.

Sikhanyiso Ndlovu Waziri wa habari wa Zimbabwe amesema kuwa watu hao walishughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, na kwamba walikuwa magaidi.