LONDON: Tony Blair anapanga mkutano wa kimataifa juu ya itikadi kali ya kiislamu
21 Julai 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Uingereza Bwana Tony Blair anapanga kufanya mkutano wa kimataifa juu ya itikadi kali ya kiislamu, kufuatia mashambulio ya Julai saba mjini London. Kiongozi huyo amesema ipo haja ya jamii ya kimataifa kushirikiana na kubadilishana mawazo katika juhudi za kupambana na ugaidi wa kimataifa.
Blair amesema mataifa 26 yameathiriwa na mashambulio ya kundi la al-Qaeda tangu mwaka wa 1993. Amesisitiza kuwa na imani na vyombo vya usalama nchini Uingereza hata licha ya mashambulio hayo ya London.