1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Tetesi zapamba moto nchini Uingereza, kuhusu mazingira ilimotokea ajali ya gari iliyosababisha kifo cha Diana

6 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlb
Kesi kuhusu kifo cha marehemu dayana binti mfalme wa Walles, kilichotokea mwaka wa 1997 kutokana na ajali ya barabarani; kesi ambayo ilikua ianzishwe leo hii mjini London, imeahirishwa hadi zaidi ya mwaka mmoja ujao.

Mwendesha mashataka anaehusika na maswali ya kisheria ya watu wa familia ya ukoo wa kifalme nchini Uingereza, Bwana Michael Burgess, amesema hata hivo, kwamba ameipelekea polisi ombi la kuanza kuchunguza ripoti ya idara za usalama za Ufaransa kuhusu ajali iliyosababisha kifo cha Diana.

Kesi ya rafiki yake Diana, hayati Dodi Al Fayed ambae kafariki pia katika ajali hiyo, ilitarajiwa kuanzishwa jioni hii-

Hii inafuatia tetesi zilizopamba moto katika vyombo vya habari nchini Uingereza, zinazotokana na kitabu kilichoandikwa na mtu aliekua mfanyakazi wa nyumbani kwake Diana, akidai marehemu alikuwa akihofia maisha yake, kabla ya ajali iliyotokea Ufaransa, na kwamba huenda ajali hiyo iliandaliwa makusudi.