1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Shirika la Amnesty International latoa ripoti ya mwaka

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz8

Shirika la kimataifa la kupigania haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti yake ya mwaka hii leo. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini London Uingereza limezitaka serikali zikatae siasa za uoga na kuwekeza katika taasisi za haki za binadamu ili kuendeleza utawala wa sheria katika ngazi ya kitaifa na kimatiafa.

Shirika la Amnesty International limeorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi zaidi ya 150 duniani, likizingatia sana ufisadi na umaskini barani Afrika.

Ripoti ya shirika hilo pia imeyashutumu maeneo yanayokabiliwa na mizozo yakiwemo Palestina, Sudan, Afghanistan na Irak.

Ujerumani imeshutumiwa kwa kuhusika kuwasafirisha kisiri washukiwa, wakati washukiwa wa ugaidi waliposafirishwa kwa njia ya siri katika nchi kadhaa na shirika la ujasusi la Marekani, CIA. Tabia ya shirika hilo imeelezwa kuwa utandawazi wa ukiukaji wa haki za binadamu.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Israel na walowezi wa kiyahudi wamelaumiwa na shirika la Amnesty International kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu wakati wa vita vya Lebanon mnamo mwaka jana.