1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON. Serikali ya Tony Blair katika mtihani mkubwa juu ya sheria ya kuwazuia washukiwa wa ugaidi

9 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEK8

Bunge la Uingereza linatarajiwa kuupigia kura mswaada utakao wawezesha polisi nchini humo kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa muda wa siku 90 bila ya kuwafikisha mahakamani.

Wapinzani wa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ndani ya chama chake cha Labour wanasema kuwa hatua hiyo itakiuka haki za binadamu na hivyo wanapanga kuupinga mswaada huo.

Kura hiyo inauweka utawala wa Tony Blair katika mtihani mkubwa.

Waziri mkuu wa Uingereza anasema kwamba hatua hiyo inaamabatana na sera za serikali yake za kupambana na vitendo vya kigaidi.

Vile vile hatua hizo zinatarajiwa kuwasaidia polisi kupambana na vitisho vipya baada ya shambulio la kigaidi mjini London la mwezi julai ambako watu zaidi ya 50 waliuwawa.