1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Pakistan yalaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu

29 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7m

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeilaumu Pakistan kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika juhudi zake za kuinga mkono Marekani kwenye vita dhidi ya ugaidi wa kimatiafa.

Shirika hilo linasema mamia ya wapakistan na raia wa kigeni walioshukiwa kuwa magaidi wamepotea na wafungwa wamekuwa wakiuzwa kwa Marekani na wawindaji wa watu kwa kiwango cha dola 5,000 za kimarekani kwa kila mfungwa mmoja.

Wengi hawajulikani waliko akiwemo kijana wa miaka 13 raia wa Saudi Arabia. Washukiwa 300 waliachiliwa na Marekani kutoka jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba, bila kufunguliwa mashtaka. Shirika la Amnesty International linasema wafungwa wengi walipelekwa Bagram nchini Afghanistan.

Ripoti ya shirika la Amnesty International imetolewa baada ya wizara ya ulinzi ya Uingereza kudai kwamba shirika la ujasusi la Pakistan, linaviunga mkono kisiri vyama vya kiislamu.

Madai hayo yamefutiliwa mbali kwa hasira na rais wa Pakistan, Pervez Musharaf.