LONDON: Misaada zaidi yapelekwa nchini Niger
28 Julai 2005Msaada wa dharura wa tani zaidi ya 40 za chakula na mahitaji mengine muhimu unatarajiwa kuwasili nchini Niger kwa ajili ya mamilioni ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame.
Msaada huo umetolewa na idara ya Uingereza inayoshughulikia maendeleo ya kimataifa. Uingereza imeahidi kutenga pauni milioni tatu kwa ajili ya kuwasaidia watu milioni tatu na laki sita wa Niger ambao sasa wanakabiliwa na hatari ya kufa njaa.
Ndege ya shirika la chakula duniani, WFP pia ipo njiani kupeleka msaada wa tani 80 nchini Niger.
Wakati huo huo shirika la misaada OXFAM la Uingereza limeutaka Umoja wa Mataifa utenge mfuko wa dharura wa dola bilioni moja ili kuweza kukabiliana na majanga ya njaa kwa haraka yanapotokea.
.