1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London: Marekani,Ufaransa zaunga mkono jumuiya za upinzani Lebanon.

1 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaN

Mawaziri wa nchi za nje wa Marekani na Ufaransa wameeleza kuwa nchi zao zinaiunga mkono jumuiya ya upinzani nchini Lebanon kufuatia kujiuzulu kwa serikali ya waziri mkuu Omar Karami .Katika tamko lao la pamoja mjini London bibi Condoleeza Rice wa Marekani na mfani wake wa Ufaransa bwana Michel Barnier pia wamesisitiza ulazima wa Syria kuondosha majeshi yake kutoka Lebanon.

Wakati huo huo tume ya Umoja wa Ulaya imesema kwamba uchaguzi wa bunge lazima ufanyike nchini humo katika mwezi wa mei kama ilivyopangwa.

Nchini Lebanon kwenyewe ghasia kubwa zimetokea katika sehemu ya kaskazini ambapo watu wanaomwuunga mkono bwana Omar Karami walishambulia nyumba za wapinzani.

Habari zinasema mtu mmoja aliuawa kutokana na ghasia hizo katika mji wa uzawa wa bwana Karami, Tripoli.