LONDON: mabadiliko ya hali ya hewa yatishia juhudi za kuondoa umasikini barani Afrika
29 Oktoba 2006Matangazo
Wawakilshi wa mashirika ya mazingira na maendeleo wamesema kwamba bara la Afrika linakabiliwa na maafa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na huenda hali hiyo ikavuruga juhudi za kuondoa umasikini.
Wawakilishi hao wamesema mjini London ,kuwa hatua za haraka lazima zichukuliwe na jumuiya ya kimataifa .
Mkuu wa utafiti kwenye shirika la misaada, Oxfam Duncan Green amesema kwamba mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanayotokea barani afrika yanawaathiri hasa watu masikini. Bwana Green ameeleza kuwa athari hizo ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga.