London. Kundi la kigaidi lililohusika la shambulio la Madrid mwaka jana limesema limehusika pia na shmabulio la London.
9 Julai 2005Matangazo
Kundi la kigaidi ambalo lilidai kuhusika na shambulizi la bomu katika treni mjini Madrid mwaka 2004 limesema kuwa pia linahusika na mashambulio ya mjini London siku ya Alhamis.
Kikosi cha Abu Hafs al-Masri kilitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Internet.
Mara baada ya mashambulio ya Alhamis, kundi jingine linalojiita kundi la siri la al Qaeda katika bara la Ulaya , pia lilidai kuhusika na lilitoa taarifa yake pia kupitia mtandao wa Internet. Ukweli wa taarifa zote hizo mbili bado haujathibitishwa.