1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Khofu kuwa haki za binadamu zimekiukwa

28 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3T

Shirika linalotetea haki za binadamu duniani,Amnesty International,linataka kupeleka tume yake nchini Lebanon kuchunguza ikiwa haki za binadamu zimekiukwa.Msemaji wa shirika hilo amesema,wote Israel na Hezbollah wana makosa ya kutumia nguvu kupita kiasi.Shirika hilo vile vile limetoa mwito wa kusita kutumia mabomu yanayotawanyika.Kwa upande mwingine,misaada ya dharura ya Shirika la Msalaba Mwekundu imewasili Lebanon,ambako kuna wasi wasi kuwa katika vijiji vingi upo upungufu wa maji na chakula.Kiasi ya wakimbizi elfu 30 wamekusanyika vijijini karibu na mpaka wa Israel na Lebanon.Halmashauri ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imeripoti kuwa hali ya afya,maji na chakula katika maeneo ya ndani,kusini mwa Lebanon ni ya kutia khofu.Tawi la Ujerumani la Msalaba Mwekundu linatuma chakula cha watoto katika eneo hilo.