1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Blair hataruhusiwa kukanyaga Lebanon

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIX

Waziri mkuu wa Uingereza, bwana Tony Blair, hataruhusiwa kukanyaga nchini Lebanon ikiwa atataka kuitembea nchi hiyo wakati wa ziara yake ya Mashariki ya Kati, ambayo iko katika hatua za mwanzo za maandalizi.

Kiongozi wa Hezbollah nchini Lebanon, Ghaleb Abu Zeinab, ameliambia gazeti la The Times akiwa mjini Beirut kwamba Blair hatakiwi nchini Lebanon.

Abu Zeinab amesema hazungumzi kwa niaba ya Hezbollah pekee bali kwa niaba ya walebanon wote ambao hawataki mtu anayelia machozi ya mamba aitembelee nchi yao.

Afisa huyo wa Hezbollah amemuita Blair muuaji wa taifa zima la Lebanon, kwa kumuunga mkono rais George W Bush wa Marekani kukataa kuitisha kwa haraka usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hezbollah kusini mwa Lebanon.