LOME: Mamia ya Watogo wakimbilia Benin na Ghana kufuatia ghasia kaskazini mwa Togo
28 Aprili 2005Matangazo
Hali ya mambo imechukua mkondo mpya nchini Togo ambapo Mamia ya watu kutoka kaskazini mwa Togo wanakimbilia nchi jirani ya Benin na Ghana kufuatia mapambano kati ya vijana na vikosi vya usalama.
Duru za Hospitali zimearifu takriban watu 22 wameuwawa na wengine 100 wamejeruhiwa katika mapigano yaliyozuka baada ya kutangazwa Faure Gnassingbe kuwa mshindi katika matokeo ya uchaguzi wa rais wa jumapili.
Wakati huo huo mgombea wa rais wa chama kikuu cha upinzani Emmanuel Akitani Bob pia amejitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais.
Hata hivyo tangazo la Akitani limepingwa na Umoja wa Afrika na jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS na kutoa wito kwa vyama vyote kumaliza mzozo na kuunda serikali ya muungano.