1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lissu afutiwa mashtaka dhidi yake

George Njogopa (HON)22 Septemba 2021

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania  imeanza kuchukua mwelekeo mpya kwa kesi zilizochukua muda mrefu mahakamani ambapo siku ya Jumatano imemfutia mashtaka kiongozi wa chadema, Tundu Lissu na wenzake watatu waliokuwa wakikabilisha na mashtaka ya uchochezi. George Njogopa ameandaa taarifa zaidi kutoka Dar es Salaam. Sikiliza.

https://p.dw.com/p/40fSL

Tundu Lissu na wenzake watatu, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano yanayohusiana na uchochezi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2016 kupitia gazeti la Mawio ambalo hata hivyo baadaye lilifutiwa ujasili wake na serikali.

Lissu kurejea Tanzania kudai katiba mpya

Mbali na Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, washtakiwa wengine walikuwa ni wahariri wa gazeti la Mawio, Jabiri Indrissa na Simon Mkina na mchapishaji wa kampuni ya Jamana Ismail Mehboo.

Walituhumiwa kuandika habari za uchochezi ikiwa ni kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002. Habari iliyowaingiza matatani ni ile iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema “Machafuko yaja Zanzibar”.  

Kesi ya Tundu Lissu yaahirishwa

Kufuatia hatua hiyo ya kufutiwa mashtaka hayo, Dw ilitaka kupata maoni kutoka miongoni mwao, na ilifanikiwa kuzungumza na mhariri wa gazeti la Mawio na alikuwa na haya ya kusema.

Hoja za kufuta kesi dhidi ya washtakiwa Tanzania zina uzito?

Mfumo wa sheria nchini Tanzania umekuwa ukokosolewa vikali hasa kutokana na vipengele vinavyonyima dhamana kwa watuhumiwa wa makosa kama ugaidi, uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha. Hali hiyo imefanya watuhumiwa wengi kusota gerezani kwa miaka mingi na hata wale wanaoachiwa huondoka mikono mitupu bila fidia.

Rais wa zamani wa chama cha wanasheria cha Tanganyika Law Society, Dr Rugemeleza Nshala ni miongoni mwa wale wanaoona kwamba sheria hiyo imepitwa na wakati.Kesi ya Lissu dhidi ya spika Ndugai yaanza kusikilizwa mahakama kuu

Katika mfululizo wa kuzifuta kesi zilizoendeshwa kwa muda mrefu,  ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ilimwachia huru wiki iliyopita mfanyabiashara wa siku nyingi, James Rugemalila aliyesota mahabusu kwa miaka minne alikokuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alitoa wito wa kufutwa kwa kesi ambazo serikali inaona haina ushahidi wa kutosha au haina mwelekeo wa kushinda. Alilitaka pia jeshi la polisi kutokuwa na haraka ya kupeleka kesi mahakamani ambazo ushahidi wake ulikuwa bado haujakamilika.