Lisbon. Matatizo ya hali ya hewa yapungua katika Ulaya ya kati.
26 Agosti 2005Matatizo ya hali ya hewa yaliyoikumba Ulaya yameanza kupungua jana wakati moto ulipoweza kudhibitiwa nchini Ureno na mafuriko yamepungua katika eneo la kati la Ulaya.
Moto uliokuwa ukiwaka nchini Ureno umewauwa watu 15, ikiwa ni pamoja na watu 10 kutoka katika jeshi la kuzima moto hadi sasa , wakati mafuriko makubwa nchini Ujerumani, Austria, Uswisi na Romania yamesababisha vifo vya watu 41.
Kwa siku nzima helikopta 14 za jeshi la Austria zilichukua chakula na madawa kwa ajili ya watalii 5,000 waliokwama katika eneo la Tyrol.
Mafuriko hayo pia yamezusha ongezeko la idadi ya matetemeko ya ardhi, kwa mujibu wa idara ya uchunguzi wa matetemeko ya ardhi nchini Uswisi.