Ligi ya mabingwa barani Ulaya AC Milan yapigwa mwereka.
4 Oktoba 2007Katika pambano hilo, shabiki mmoja wa Celtic, aliingia uwanjani baada ya Scott McDonald kuipatia timu hiyo kupata bao la ushindi katika dakika ya 90, ambapo alimkimbilia mlinda mlango wa AC Milan Dida na kumpiga kijikofi.Dida alimkimbiza kwa umbali mfupi na baadaye kuanguka chini ambapo ilibidi atolewe kwa machela.
Shirikisho la soka la Ulaya limesema kuwa linasubiri ripoti ya kamisaa kabla ya kuiadhibu Celtic.
Katika mechi nyingine Liverpool ililambishwa mchanga nyumbani na Olympique Marceille baada ya kuchapwa bao 1-0, huku Porto ikipata ushindi kama huo ugenini dhidi ya Besiktas ya Uturuki
Schalker 04 ikicheza ugenini ilifuta machozi ya wajerumani kwa timu zao kufanya vibaya katika champions league baada ya kuichapa Rosenburg mabao 2-0, mabao yaliyowekwa wavuni na Kevin Kuranyi na Jermaine Jones yote katika kipindi cha pili.
Timu nyingine ya Ujerumani Bremen ikiwa nyumbani hapo jana ilizabwa mabao 3-1 na Olympiakos ya Ugiriki.
Bremen ilikuwa ikiongoza kwa bao 1 hadi zilpobaki dakika 17 mpira kumalizika wakaishiwa nguvu na kutoa mwanya kwa wagiriki kupachika mabao 3 ya haraka haraka.
Katika mechi nyingine Chelsea waliibuka kutoka usingizini na kuichapa Velencia nyumbani mabao 2-1 baada ya kuwa nyuma kwa bao 1.
Ushindi huo umeamsha morali mpya kwa timu hiyo iliyokuwa bado na jinamizi la kuondokewa na kocha wake Jose Morinho.
Mabao mawili Ruud Van Nestroy yalisaidia Real Madrid kulazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Lazio.
Jioni hii timu kadhaa zinaingia uwanjani katika mechi za kombe la UEFA ambapo Buyern Munich ya Ujerumani inakumbana na Belenenses, huku Hamburg ikiwa nyumbani kuwaalika Lovech. Timu nyingine ya Ujerumani Nurenberg inakaribishwa mjini Bucharest Romania na Rapid.