Ligi kuu ya kandanda England yapamba moto
16 Februari 2016Na kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anaweza kukabiliwa na hatua kali kutoka chama cha soka nchini Uingereza baada ya raia huyo kutoka Chile kumkosoa refa Mark Clattenburg baada ya timu yake kushindwa hapo jana dhidi ya Tottenham.
Pellegrini alimshutumu refa Clattenburg kwa kutaka kuwazawadia penalti Spurs na kutoa tathimini kali dhidi ya refa huyo kutokana na jinsi alivyoendesha mchezo mwingine na Tottenham mwezi Septemba mwaka jana.
Kikosi cha kocha nyota Juergen Kloop cha Liverpool kiliirarua Aston Villa jana Jumapili kwa mabao 6-0 na kuimarisha nafasi yake kuelekea katika nfasi za kucheza kombe la Ulaya.
Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae /zr /
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman