Libya yawakamata wahamiaji 948
25 Juni 2018Matangazo
Operesheni hizo zilizoanza tangu wiki iliopita, zinafikisha idadi jumla ya wahamiaji hasa wa Kiafrika wanaojaribu kuvuka bahari kwenda Italia lakini wakarejeshwa Libya kuwa karibu 2,000.
Pwani ya magharibi ya Libya ndio njia kuu ya kuondokea kwa maelfu ya wahamiaji wanaokimbia vita na umaskini na kujaribu kuingia barani Ulaya.
Msemaji wakikosi cha jeshi la majini la Libya, Ayoub Qassem, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa walinzi wa pwani waliwakamata wahamiaji haramu katika makundi tofauti.
Kundi la kwanza lilikuwa na watu 97 na la pili lilikuwa na wahamiaji 361, wakiwa kwenye boti za mipira.