Libya magharibi, yatishia kuzuia usafirishaji mafuta
25 Juni 2023Hamad ameidai serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa ya mjini Tripoli inapoteza mapato ya nishati.
Katika taraifa yake kiongozi huyo amesema kwamba "amezuia mapato ya mafuta ya mwaka 2022 " zaidi ya dinari bilioni 130 ambazo ni karibu dola za kimarekani bilioni 27 kama hatua ya kwanza.
Soma pia: Libya yafikia makubaliano ya mafuta na gesi na Italia
Taarifa hiyo imeeleza kwamba serikali ya mashariki mwa Libya haitambui mamlaka ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli, na iko tayari kwa hatua zaidi, ikiwa ni pamoja na kuzuia mafuta, na itatafuta uamuzi wa kisheria.
Hamad ameishutumu serikali ya Tripoli kwa kupoteza fedha za nishati kwa kile alichokuitaja kuwa ni ""matumizi makubwa kupita kiasi", bila kufafanua zaidi.
Libya ni nchi yenye hifadhi kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika, lakini imekumbwa na mzozo tangu ulipotokea uasi ulioungwa mkono na jumuiya ya kujihami ya NATO uliomuangusha aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Moamer Gadhafi mwaka 2011.