Lewandoski na Gnabry nje dhidi ya PSG
7 Aprili 2021Lewandowski ataikosa mechi ya leo ya robo fainali kutokana na jeraha la goti alilopata wakati akichezea timu yake ya taifa ya Poland, huku Gnabry akiikosa mechi hio baada ya kuambukizwa virusi vya Corona. soma zaidi Pigo kwa Poland na Bayern baada ya Lewandowski kupata jeraha
Kocha wa Bayern Munich Hansi Flick huenda akalazimika kumchezesha aliyekuwa mshambuliaji wa PSG Eric-Maxim Choupo-Moting kuziba pengo la Lewandowski.
Safu ya ulinzi ipo imara
Katika safu ya ulinzi, Hansi Flick ana wachezaji wa kutosha kabisa hasa baada ya Jerome Boateng na Alphonso Davies kurudi dimbani baada ya kuwa nje kufuatia marufuku.
Kutokana na kasi aliyo nayo Alphonso Davies, anaweza kuchukua nafasi ya Lucas Hernandez huku Jerome Boateng akiwa na fursa kubwa ikilinganishwa na Niklas Sule ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha lakini sasa ameanza kuimarika kimchezo. Lewandowski hafikirii kustaafu
Chelsea na FC Porto
Vile vile leo usiku FC Porto itachuana na Chelsea katika kinyanganyiro hicho cha Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Christian Pulisic na N`Golo Kante watajumuisha katika kikosi cha leo baada ya kupona majeraha.
Mshambuliaji Tammy Abraham atajumuisha katika kikosi cha leo baada ya kuachwa nje katika mechi ya ligi kuu England walipopokea kipigo cha mabao 5-2 kutoka mikononi mwa vimbonde West Bromwich.
Hata hivyo kuna uwezekano kuwa wa N'Golo Kante huenda akakosa kuanza katika mechi hii baada kulalamika hivi karibuni juu ya maumivu ya misuli.
FC Porto itakosa huduma za kiungo Sergio Oliveira ambaye anatumikia marufuku. Oliviera alifunga mabao mawili na kuisaidia Porto kufuzu dhidi ya Juventus katika raundi ya 16 bora.
Klabu hii ya Ureno pia itamkosa Mehdi Taremi, ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi ya marudiano dhidi ya Juventus.
AP