Leo siku ya kimataifa ya kupiga vita kufanyishwa kazi watoto
12 Juni 2006Katika nchi za Kiafrika watoto wengi zaidi wanafanya kazi, yaani karibu kila mtoto wa tatu. Kwenye siku ya kimataifa hii leo ya kupiga vita kufanyishwa kazi watoto, shirika la UNICEF linalojihusisha la jambo hilo, linalaumu hali hiyo mbaya.
Kwa mwenyekiwanda kuwaajiri watoto humpatia mapato makubwa. Kwanza wanakubali mishahara midogo na kwa vile hawana chama cha wafanyakazi hawawezi kupinga saa ndefu ya kufanya kazi. Sababu zinazowabidii watoto waende kutafuta kazi ni nyingi. Hasa wanazisaidia familia zako. Kutokana na vita na kuenea ugonjwa wa ukimwi katika nchi za Kiafrika, watoto wengi wanajitegemea.
Matokeo ya kufanya kazi katika umri wa utoto ni mabaya sana, anasema Helga Kuhn, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mambo ya watoto, UNICEF: “Aina ngumu za kazi watoto ambazo shirika la UNICEF linataka kuziondoa haraka sana zinaathiri afya za watoto hawa. Kazi inaweza kuwa ngumu sana, kwa mfanok kubeba mizigo mizito ama watoto wanakaa kwa njia fulani kwa muda mrefu wakifuma mazulia. Lakini tatizo kuu ni kwamba watoto hawa hawawezi kwenda shuleni. Hivyo wanauharibu mustakabali wao.”
Umaskini ndio sababu kuu ya watoto kufanya kazi, lakini pia umaskini ni matokeo yake. Ikiwa watoto wa familia maskini wanafanya kazi, hawawezi kwenda shula na hivyo watabaki kuwa maskini baadaye katika maisha yao. Hawatakuwa na elimu ya kutosha ili kuwahudumia jamaa zako, na hivyo tena hawataweza kuwapeleka watoto wao shuleni.
Kazi ya watoto lakini ni tatizo la utandawazi, kwani bidhaa zilizotengenezwa na watoto zinanunuzwa na kununuliwa katika nchi tajiri. Kwa hivyo, wanunuzi pia wanasababisha kazi ya watoto iendelee. Tayari makampuni mengi ya kimataifa yalijiwekea masharti maalum kutowaajiri watoto katika viwanda vyao vilivyopo nchi zinazoendelea. Hata hivyo, makampuni haya hayawezi kuzuia kampuni zao nyingine ndogo ndogo zisiwaajiri watoto.
Kwa mujibu wa shirika la UNICEF, katika miaka kadhaa iliyopita, limeweza kufanikiwa kidogo katika kupiga vita kazi ya watoto. Nchi nyingi zilikubali masharti yaliowekwa ya shirika la wafanyakazi duniani, ILO juu ya umri wa chini wa wafanyakazi. Lakini inabidi pia serikali za nchi hizo ziweke sheria maalum ili masharti haya yatekelezwe. Kwa hivyo shirika la UNICEF linataka shirika la ILO liweke vikwazo vya kiuchumi, kama linavyofanya shirika la biashara duniani, WHO, ikiwa nchi fulani hazitekelezi masharti yake juu ya kazi za watoto.