1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LEIPZIG:Chama cha CDU chakamilisha mkutano wake

3 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvm
Hapa nchini Ujerumani chama cha upinzani cha Christian Demokratic Union kimekamilisha mkutano wake mkuu wa kila mwaka mjini Leipzig. Kiongozi wa chama hicho cha CDU Angela Merkel amewaambia wajumbe kwamba mkutano huo umewaonyesha wapiga kura wa Ujerumani kwamba chama hicho ni mbadala unaofaa kwa chama cha Social Demokrat kinachoongoza serikali cha Kansela Gerhard Schroeder.Wajumbe wa chama hicho wameidhinisha mpango wenye mapendekezo makubwa yanayokusudia kuufanyia mageuzi uchumi wa Ujerumani na mfumo wa ustawi wa jamii.Wanaounga mkono mapendekezo hayo wanasema utapunguza gharama za watu wasiolipwa mishahara pamoja na kutowa nafasi za ajira. Chama cha Social Demokrat kimeshutumu mapendekezo hayo kwa kusema kwamba yatamaanisha kumalizika kwa mfumo wa ustawi wa jamii nchini Ujerumani.