1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Leicester yashuka, Everton yaponea

29 Mei 2023

Miaka saba baada ya Leicester City kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England, klabu hiyo imeshushwa daraja baada ya kumaliza msimu katika nafasi ya 18.

https://p.dw.com/p/4RwAe
Jamie Vardy von Bramall Lane Leicester City bricht eine Eckfahne
Picha: Jason Cairnduff//PA Images/imago images

Leicester walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham United hapo jana ila Everton wakapata ushindi wa 1-0 walipokuwa wakicheza na Bournemouth na wakawapiku na kuichukua nafasi ya 17 katika msimamo.

Kocha wa Everton Sean Dyche lakini anasema kuna mengi yanayostahili kufanywa katika klabu hiyo ili kuirejesha pale ilipokuwa kimchezo na isijikute katika hali sawa na hii ya kupigania kusalia katika ligi msimu ujao.

"Tatizo kubwa kuhusu Everton tangu nilipokuja hapa ni mtazamo mbaya kuhusiana na kila kitu, kwa hiyo nilijaribu na kubadilisha hilo. Ni vigumu si rahisi ila habari njema ni kwamba tumekamilisha kazi, wachezaji wamefanya kazi yao bila shaka. Nimekuja kubadilisha mitazamo na nafikiri kumekuwa na ishara ya hilo ila bado kuna mengi ya kufanywa," alisema Dyche.

Wengine walioungana na Southampton kushuka daraja ni Leeds United ambao licha ya kuwa nyumbani walicharazwa magoli 4 kwa moja na Tottenham Hotspur ambapo mshambuliaji Harry Kane alifunga mabao mawili katika mechi hiyo.

Kocha Sam Allardyce ambaye aliajiriwa kuelekea mwishoni mwa msimu ili ainusuru klabu hiyo isishuke, alikuwa na haya ya kusema.

"Sijafurahia wakati wangu kama kocha wa Leeds, nina furahi nilirudi kuwa meneja na nikajaribu kadri ya uwezo wangu kuiondoa klabu hii katika matatizo kwasababu siwezi kufurahia chochote kama sishindi, huyo si mimi. kwa hiyo tumevunjika moyo pakubwa," alisema Allardyce.