Lebanon yakabiliwa na mzozo wa kisiasa
23 Novemba 2007Matangazo
Lebanon inakabiliwa na mzozo wa kisiasa baada ya upande wa upinzani unaoungwa mkono na Syria kutishia kuwa hautoshiriki kumchagua rais mpya.Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Uhispania na Italia waliokuwa wakijaribu kuleta maafikiano kati ya pande mbili nchini Lebanon, sasa hawana matumaini ya kufanikiwa.
Kuna hofu kuwa hali hiyo huenda ikazusha upya machafuko ya kimadhehbu,kama ilivyokuwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 15.Vita hivyo vilimalizika mwaka 1990.