Lebanon kuzuwia kuvunja mapatano
20 Agosti 2006BEIRUT:
Serikali ya Lebanon imeapa kuzima jaribio lolote kutoka Lebanon kuvunja mapatano ya kuacha mapigano yaliofikiwa na Israel.Waziri wa ulinzi Elias al-Murr ameuwambia mkutano wa waandishi habari hii leo, jeshi litachukua hatua kali kukandamiza ukiaukaji wowote wa m apatano hayo.Aliarifu pia kwamba, jeshi la Lebanon linadhibiti sasa eneo la mpakani na Syria n a litazuwia shehena zozote za silaha kuingia Lebanon.
Nae waziri wa nje wa Lebanon Fwzi Sallukh amesema mjini cairo kwamba nchi yake iliovurugwa kwa vita inatumai kupata msaada zaidi wa kujenga upya kutoka nchi nyengine za kiarabu.Akasema kwamba, anatumai nchi za kiarabu zitapitisha azimio hii leo kuiungamkono Lebanon.Waziri wa nje wa syria,walid Muallem hatahudhuria kikao cha Kairo.