1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Le Graet kikaangoni Ufaransa kuhusu Zidane

9 Januari 2023

Rais wa shirikisho la kandanda Ufaransa Noel Le Great ameomba radhi kwa kile alichokiita matamshi yake yasiyo na heshima kuhusu uwezekano wa Zinedine Zidane kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4LuZH
Kombobild | Noel Le Graet und Zinedine Zidane
Picha: Christophe Ena/AP/Francois Mori/AP/dpa

Le Great mwenye umri wa miaka 81 alifanya mahojiano na redio moja ya Kifaransa akisema kuwa hata asingeweza kupokea simu ya Zidane, wakati alipoulizwa kama Zidane angempigia simu kuelezea nia ya kumrithi Didier Deschamps kama kocha wa Les Bleus.

Hiyo ilizusha ukosoaji kutoka kwa nyota wa Ufaransa na Paris Saint-German Kylian Mbappe aliyeyaita matamshi ya La Graet kuwa yasiyo na heshima.

Waziri wa michezo wa Ufaransa Amelie Oudea-Castera aliingilia akimtaka Le Graet aombe radhi kutokana na matamshi hayo ambayo alisema ni aibu nay a kukosha heshima.

Deschamps alisaini mkataba mpya hadi Kombe la Dunia la mwaka wa 2016 baada ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa walishindwa na Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia la Qatar kupitia mikwaju ya penalti.