1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAMPEDUSA: Wahamiaji wengine zaidi ya 400 kutoka Afrika waingia nchini Italy

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzw

Wahamiaji zaidi ya 400 wamefika katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italy. Wahamiaji hao ambao inadhaniwa ni kutoka Afrika, wamewaita walinzi wa pwani kwa kutumia simu za mkononi na hivyo kuokolewa umbali wa kilomita kiasi ya 10 kutoka pwani. Hadi sasa haijajulikana uraia wa wahamiaji hao lakini inaaminiwa wamepitia nchini Libya. Taarifa zingine zinasema wahamiaji wengine 29 wameokolewa katika kisiwa cha Canary nchini Hispania. Viongozi nchini Hispania wanasema idadi ya wahamiaji iliongezeka mara mbili ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka uliopita.