1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAMPEDUSA. wahamiaji haramu waingia Italia

29 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEgf

Wahamiaji 500 wameingia nchini Italia kupitia fuo za pwani za Sicily na Lampedusa na wengine huko Crete pwani ya Ugiriki.

Baadhi ya wahamiaji 150 kutoka Afrika Mashariki na Afrika Magharibi walipelekwa hospitali mara tu mashua yao ilipotua nanga katika kisiwa cha Sicily kutokana na hali mbaya ya afya na uchofu wa safari ndefu.

Polisi katika kisiwa cha Lampedusa wamewakamata washukiwa wawili wa biashara ya kuwaingiza watu kinyume cha sheria.

Habari zaidi zinaarifu, kwamba biashara aina hiyo hufanyika zaidi wakati wa msimu wa kiangazi licha ya juhudi zinazo fanywa na bara Ulaya kumaliza uingizaji watu kiharamu.

Walinda usalama wa baharini wa Italia wamesema watuhumiwa hutumia mashua ndogo ndogo ili kukwepa kuonekana kwa urahisi na vyombo vya usalama wa baharini.