SiasaTaiwan
Lai Ching-te asema yuko tayari kufanya kazi na China
26 Mei 2024Matangazo
Lai amewaambia waandishí wa habari mjini Taipei kuwa anataka Taiwan na China "kubeba kwa pamoja jukumu la kuhakikisha utulivu wa kikanda."
Kiongozi huyo ameendelea kueleza kuwa, anapania kuimarisha maelewano na ushirikiano na China kuelekea kupatikana kwa amani na ustawi wa pamoja.
Soma pia: Luteka za jeshi la China karibu na Taiwan zimemalizika
Mnamo siku ya Alhamisi, China ilifanya luteka za kijeshi katika eneo linaloizunguka Taiwan, siku tatu tu baada ya Lai Ching-te kuapishwa, luteka hizo zikichukuliwa kama kampeni inayoongezeka ya vitisho kwa Taiwan, ambayo China inakiona kisiwa hicho kama sehemu ya himaya yake.
Wakati wa luteka hizo za kijeshi, China iliapa kuwa "vikosi huru" vitaachwa huku vichwa vyao vimevunjika na damu inamwagika."