1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS:Uamuzi wa kutoialika Zimbabwe haukuwa rahisi

1 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFwH
Uamuzi wa Nigeria wa kutoialika Zimbabwe katika mkutano ujao wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola mjini Abuja Nigeria hakukuwa rahisi kufikiwa. Hayo yameelezwa na Rais Olesegun Obasanjo wa Nigeria.Katika mahojiano yaliofanyika moja kwa moja kwenye televisheni Obsanjo amesema haukuwa uamuzi rahisi na anaamini ingelikuwa sio sahihi kuialika Zimbabwe kuliko kutoialika nchi hiyo na kwamba angelipendelea kuwa kwenye upande wa kutoialika Zimbabwe. Obasanjo amesema uamuzi wa kutoialika Zimbabwe katika mkutano huo unaotazamiwa kuanza Ijumaa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kwa kiasi kikubwa umetokana na kushindwa kukubaliana juu ya suala la Zimbabwe kwa nchi tatu za Jumuiya ya Madola zilizochaguliwa kuliangalia suala la Zimbabwe. Baraza la nchi hizo tatu za Jumuiya ya Madola linawajumuisha pamoja Obasanjo,Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Waziri Mkuu wa Australia John Howard. Obasanjo amesema mkutano huo pia utajadili kusitishwa uwanachama wa Zimbabwe kwenye jumuiya hiyo.