LAGOS: Raia wa Italia aachiwa huru nchini Nigeria
18 Januari 2007Matangazo
Wanamgambo wa Nigeria wamemwachia huru mfanyikazi wa kampuni ya mafuta, raia wa Italia anayeugua waliyemteka nyara kiasi mwezi mmoja uliopita.
Roberto Dieghi pamoja na wafanyikazi wenzake watatu wa kampuni ya Agip walitekwa nyara majuma sita yaliyopita na kundi linalotetea jimbo la Niger Delta kujitenga.
Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya Italia imethibitisha kuwa Roberto Dieghi aliachiwa huru na kwamba mashauriano yanaendelea kusaidia kuachiwa huru kwa mateka waliobaki.
Siku ya jumanne iliyopita watu watatu, akiwemo raia mmoja wa Uholanzi waliuawa katika eneo hilo wakati mashua yao iliposhambuliwa.