1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagos. Fedha zilizoibwa na dikteta Abacha zimerejeshwa zatumika katika mradi.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgx

Serikali ya Nigeria imetumia fedha zilizochotwa na dikteta wa zamani wa nchi hiyo marehemu Sani Abacha na kugharamia miradi ya maendeleo wakati fedha hizo ziliporejeshwa, taarifa ya benki ya dunia imesema.

Fedha hizo zilizouibiwa kutoka kwa watu wa Nigeria na dikteta wa zamani Sani Abacha , na kurejeshwa nchini Nigeria kutoka Uswisi chini ya makubaliano yaliyotiwa saini 2005, zilitumika kwa miradi ya maendeleo katika sekta tano, imesema taarifa hiyo ya benki ya dunia iliyotolewa mjini Abuja nchini Nigeria.

Mapema mwezi wa Desemba chama cha kiutu cha Uswisi, kimesema kuwa kumekuwa na matatizo katika matumizi ya fedha hizo.