1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KYOTO:Bi Merkel akamilisha ziara ya Uchina na Japan

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBU9

Kansela wa ujerumani Bi Angela Merkel yuko mjini Kyoto nchini Japan kuadhimisha miaka 10 tangu makubaliano ya Kyoto ya kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya anga kufikiwa mjini humo.Bi Merkel aliyehusika katika mazungumzo ya mwaka 97 yaliyofanikisha kufikiwa kwa makubaliano ya Kyoto ya kupunguza viwango vya gesi za viwanda analipa kipa umbele suala la mazingira kama kiongozi wa kundi la mataifa nane yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8.

Bi Merkel abatarjiwa kuhutubia mkutano unaojadilia ongezeko la joto ulimwenguni katika siku yake ya mwisho ya ziara ya wiki nzima nchini Uchina na Japan.Kiongozi huyo alikuwa mwandalizi wa mkutano wa kilele wa kundi la G8 uliofanyika mwezi Juni na kuafiki kupunguza viwango vya gesi za viwanda kw anusu ifikapo mwaka 2050.

Kundi la G8 linajumuisha pia Marekani iliyo mtoaji mkubwa wa gesi za viwanda japo inapinga makubaliano ya Kyoto kwani hayashinikizi mataifa yanayoinukia kama India na Uchina kupunguza viwango vyao vya gesi za viwanda.

Mazungumzo mengine yanapangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu mjini Bali nchini Indonesia ili kuandaa rasimu itakayofuatwa baada ya makubalino ya Kyoto kumaliza muda wake mwaka 2012.