1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini wasio Waislamu hufunga mwezi wa Ramadhan?

22 Machi 2024

Katika eneo la Mashariki ya Kati huezi kuuepuka mwezi mtukufu wa Ramadhan, kwahiyo sio kitu kigeni kwa wale wasiokuwa waislamu kufunga katika mwezi huo muhimu kwa waumini wa kiislamu.

https://p.dw.com/p/4e0T7
Bildergalerie Ramadan Fastenmonat der Muslime | Nepal, Kathmandu
Picha: Navesh Chitrakar/REUTERS

Ni nadra kwa Muislamu kusema maneno haya, lakini Kholoud Khardoum, aliye na miaka 53, anaeishi nchini Iraq yuko wazi kabisa kwamba, sio kila ramadhani inahusu dini, saa nyengine inahusu mazingira na utamaduni wa watu kuja pamoja.

Aliiambia DW kuwa Iraq ni nchi yenye waislamu wengi, lakini katika maeneo ambayo jamii mbalimbali za kidini zinaishi pamoja, mara nyingi utawakuta watu wasio waislamu wakifunga katika mwezi mtukufu wa ramadhani. Hasa, wakati wa "iftar," mlo unaoliwa wakati wa kufungua baada ya jua kuzama, ambapo familia na marafiki hukutana na kula pamoja. Hili kwa kawaida linakuwa jambo la jamii nzima.

Soma: Je, washawishi wa mitandaoni wainabadilishaje ibada ya Ramadhani?

Kholoud Khardoum ameongeza kuwa wakati mwingine wakristo hutayarisha chakula na kuwapelekea majirani zao waislamu, na saa nyengine waislamu wanawapelekea ndugu zao wakristo chakula au hata wote kufunga pamoja. Anasema inapendeza sana kuwa na umoja huo.

Bangladesh| Ramadan
Iftar mjini Dhaka BangladeshPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Mambo kama haya pia husimuliwa katika sehemu nyengine za Mashariki ya Kati. Um Amira ni raia wa Misri aliye na miaka 50 anayeishi Assiut, mji ulio kusini mwa Cairo anasema, moja ya marafiki zake wa karibu ni muislamu," kwahiyo huwa anafunga na yeye siku nzima na baadae jioni wanafungua pamoja na kula pamoja na familia ya rafiki yake.

Mfano mwengine ni wa Rita, mwanamke aliye na miaka 34 raia wa Lebanon, anayefunga pia katika mwezi mtukufu wa ramadhani, anasema yeye ni mkristo lakini tangu mdogo amekuwa na marafiki wengi wa kiislamu, na hajawahi kuweka msisitizo mkubwa katika dini tofauti.

Fuatilia: Ramadhani yaanza bila usitishwaji vita Gaza

Ikizingatiwa kuwa wanawake wote watatu wanaishi katika nchi zenye waislamu wengi, mambo wanayoyasimulia hayatawashangaza wale wanaoishi huko. Hata hivyo, ni vigumu kwa wasio waislamu kupuuza ramadhani kama ilivyo kwa waislamu kuepuka sherehe za krismasi barani ulaya au Amerika Kaskazini. lakini, Ramadhani pia polepole inaanza kuwa maarufu katika nchi zilizo na wakristo wengi.

England |  Ramadan | London
Sehemu ya mitaa ya London iliyopambwa kuwatakia Waislamu Ramadhan njemaPicha: Can Nguyen/Captital Pictures/picture alliance

Mwaka jana, London lilikuwa jiji kubwa la kwanza la ulaya kupamba sehemu ya barabara zake na taa za kupendeza na kuwatakia waislamu wote huko Ramadhani njema. Mji wa Frankfurt am Main nchini Ujerumani ulifuata mfano wa London mwaka huu, na kuwa jiji la kwanza kubwa nchini humo kuanza mfumo huo wa  kuwatakia wasialamu ramadhani njema kwa kupamba sehemu ya barabara zake kwa taa hizo maridadi.Waislamu duniani waanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Nako nchini Austria, wiki hii zaidi ya watu elfu 1,000 walikusanyika pamoja kwa ajili ya "iftari ya wazi" katika jimbo la Carinthia, ambapo jamii yote inaalikwa kula pamoja - hata kama sio waislamu na hawajafunga. Waandalizi wanasema tukio hilo huvutia watu wengi zaidi kila mwaka.

Esther-Miriam Wagner, mkurugenzi wa Taasisi ya Woolf ya Chuo Kikuu cha Cambridge, inayofuatilia mahusiano kati ya wayahudi, wakristo na waislamu, amethibitisha kwamba, "kumekuwa na ongezeko la futari zilizoandaliwa na taasisi za serikali, mashirika ya misaada na makanisa kusherehekea au kuonyesha umoja wao."

Ramadan | Pakistan, Karatschi
Iftar huko Karachi-PakistanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Farid Hafez, mtafiti mkuu katika Bridge Initiative, mradi unaochunguza chuki dhidi ya Uislamu yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Georgetown cha Washington, anasema Ramadhani pia inahusu kutambuliwa kisiasa na usawa kwa waislamu katika maeneo ya wazi.Leo ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani kwa Waislamu wengi

Biashara pia hunoga wakati huu, waislamu hutumia fedha zaidi wakati wa Ramadhani kwa kila kitu kuanzia zawadi na nguo hadi chakula na hata magari. Katika eneo la Mashariki ya Kati pekee, matumizi ya Ramadhani ya mwaka 2023 yyalizidi dola bilioni 60.

Lakini sio kila mtu anafurahishwa na utangamano uliopo kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu wakati huu wa Ramashani. Baadhi ya viongozi wa kidini hawataki walio waislamu kufunga na wale wa ulaya walio na misismamo mikali waamani hilo huenda likaharibu ustaarabu wao.