Uchaguzi mkuu wa Uholanzi unafanyika Machi 15 na siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia zinazidi kupata umaarufu. Jina moja linatawala kampeni za uchaguzi - Geert Wilders, kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, kinachoupinga Umoja wa Ulaya na Uislamu cha Freedom Party PVV.