Kikwete anaamini ni sahihi Magufuli kuikosoa serikali yake
29 Septemba 2015Viongozi wa kisiasa wa vyama mbalimbali wanaendelea na kampeini zao kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 25 Oktoba. Hadi sasa, wagombea wanaotajwa kuwa na mchuano mkali ni wale wa chama kilichoko madarakani (CCM) na wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambao ni muungano wa vyama vya upinzani - CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
Hata hivyo, kwa muda mrefu sasa, mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, amekuwa akitumia staili ya kuikosoa serikali ya chama chake kwenye kampeni zake, badala ya kutetea rikodi ya serikali hiyo inayoongozwa na Rais Jakaya Kkwete anayemaliza muda wake.
Katika mahojiano haya na meneja kampeni wa Magufuli, Abdallah Bulembo, mwandishi wetu wa Bukoba, Seif Upupu, anamuuliza meneja huyo juu ya staili hii ya kutoa lawama kwa serikali, ambayo yeye Magufuli alikuwa waziri.
Bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini kusikiliza mahojiano hayo
Mwandishi: Seif Upupu
Mhariri Mohammed Abdul-Rahman