1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuwasaidia manusura wa Ebola

Kriesch, Adrian5 Desemba 2014

Mara nyingi manusura wa ugonjwa wa Ebola huwa wanabaguliwa au kutengwa. Hakuna haja ya kuwatenga manusura wa Ebola

https://p.dw.com/p/1DzfP
Liberia Ebola Überlebende
Picha: John Moore/Getty Images

Mara nyingi manusura wa ugonjwa wa Ebola huwa wanabaguliwa au kutengwa. Manusura hawa hujikuta wapweke baada ya kutorokwa na jamaa na marafiki zao, huku wengine wakupoteza kazi zao. Kwa kweli hii si haki na ni makosa. Siku chache tu baada ya virusi hivyo kutoweka mwilini, mgonjwa hawezi tena kusambaza virusi vya Ebola, ingawa vinaweza kujificha kwenye mbegu za uzazi kwa muda wa majuma kadhaa baada mtu huyo kupona. Hivyo manusura wa Ebola wanahitajika kutumia mipira ya kondomu kila wakati wanapofanya tendo la ngono na wapenzi wao kwa muda usiopunguamajuma matatu baada ya kutoweka kwa dalili za Ebola mwilini

Damu ya manusura wa Ebola huwa na kinga ya kuzuia kuambukizwa tena ugonjwa huo baada ya kupona, na kinga hii pia inaweza kutumiwa kuwatibu wagonjwa wengine walio na virusi hivyo.

Hakuna haja ya kuwatenga manusura wa Ebola. Wanahitaji upendo na kusaidiwa kurudia maisha yao ya kawaida, kwani tayari wamepitia hali ngumu wakiugua maradhi mabaya na hata wengine kuwapoteza jamaa zao. Hivyo kikubwa wanachohitaji ni upendo na kusaidiwa ili kuwaepushia dhiki zaidi.