Kutoka Rais mpaka Shabiki - Mashujaa wa "Mia san mia"
Bayern Munich ni timu ya mpira yenye mashabiki kote ulimwenguni katika ngazi zote. Wote wanaipenda Bayern kutokana na usanii wake wa uchezaji mpira.
Uli Hoeneß(Munich) - Rais wa FC Bayern
"Siku zote nilihisi Bayern München inaongoza kutoka klabu ndogo hadi ulimwengu mzima." Kwa hiyo, yeye anafanya kazi kama meneja lakini pia ni rafiki na mshauri wa wachezaji. Kisha mwezi Machi mwaka 2014 alifungwa jela kwa miezi 11 kwa kukwepa kulipa ushuru.
Kamal Abu Lail (Nazareth, Israel) - Shabiki wa Bayern
"Bayern wakifunga bao, haijalishi ni Mpalestina au Myahudi, unamkumbatia kila mtu," alisema Kamal ambaye ni Mpalestina anayeishi Israel. Tangu miaka ya '70, amekuwa shabiki wa Bayern ambao kwa utani wanajiita 'The Bavarias'. "Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi tu na nilikuwa nawaona wachezaji kama Rummenigge, Beckenbauer, Breitner na nikaupenda mchezo wao."
Philipp Lahm (Munich) - Mchezaji wa nyumbani Munich
Philip Lahm ni bingwa wa Bayern München. Kwa karibu miongo miwili, Lahm mwenye umri wa miaka 33 amekuwa akicheza soka yake Munich lakini kwa sasa amestaafu. Lakini wakati huo huo anaonekana kama mchezaji mpya bado. "Kwa sababu nilikuwa mwembamba kuliko wenzangu, labda hilo ndilo lililonipa motisha na kufanya nifanikiwe FC Bayern."
Kanata Tokumoto (Fuchu City, Japan) - Shabiki wa Bayern
Kanata ni mwanafunzi katika shule ya mafunzo ya soka ya Tsuneishi ambayo ni ya FC Bayern katika jimbo la Fukushima. Kanata mwenye miaka 14 ni mchezaji mzuri sana kiasi cha kwamba Bayern walituma mkufunzi wa timu yao ndogo ili amtazame.
Samuel "Sammy" Osei Kuffour (Accra, Ghana) - Mchezaji wa zamani
Alitoka Ghana akiwa na umri wa miaka 17 na akapitia Italia na akaingia Munich. Uli Hoeneß alikuwa kama baba yake na alimuunga mkono wakati mambo yalipokuwa magumu kwake. Hususan baada ya kifo cha mwanawe wa kike, walitangamana vyema na ile kauli ya "Mia san Mia" ilikuwa muhimu sana kwa Mghana huyo.
Camila Borborema (Rio de Janeiro, Brazil) - Shabiki wa Bayern
Baadhi ya Wabrazili wakati mwengine husema Camila ana wazimu.Licha ya kuwa kuna vilabu vingi Brazil, Camila mwenye miaka 24 ameshikilia kuishabikia Bayern. "Oliver ndiye mtu ninayempenda, hakuna mtu mwengine duniani ninayempenda, nampenda kuliko kitu chochote kile."
Oliver Kahn (Munich) - Mlinda lango Lejendari
Baadhi ya watu wanamuita "Mkuu", wengine wanamuita "Bestia Negra" na wengine wanamfahamu kama mnyama mkali sana. Lakini wote wanakubaliana katika jambo moja: Hakuna aliye na uhusiano wa karibu na Bayern Munich kama Oliver Kahn. "Nilizikubali kanuni zote za klabu kwa sababu ufanisi unawezekana tu kupitia kutambulika na kile unachofanya," alisema mlinda mlango huyo wa zamani.
Franz "Bull" Roth (Bad Wörishofen)
Katika Fainali za Kombe la Ulaya 1967, alifunga bao la ushindi dhidi ya Glasgow Rangers katika dakika za ziada za mechi. Huu ndio uliokuwa mwanzo wa ufanisi wa Bayern Munich katika ngazi ya kimataifa. "Mlinda lango alikuwa ametoka kunikabili lakini shuti niliyoipiga ikaenda chini ya mwamba, kwa hiyo tulishinda kikombe."
Giovane Elber (Mato Grosso, Brazil) - Mchezaji wa zamani
Giovane Elber anaishi maisha mara mbili. Nchini Brazil karibu na mpaka wa Bolivia, anamiliki shamba la ng'ombe 5000. Lakini Bayern Munich wanapomuhitaji, anapatikana kwa haraka kwani anasafiri kote ulimwenguni kama balozi wa Bayern. Kwa ule msemo wa "Mia san mia" anakumbuka wakati wake akiwa mchezaji wa Bayern.
Raffael Noboa y Rivera (New York, USA) - Shabiki wa Bayern
Raphael alizaliwa Puerto Rico ila anaishi New York anakofanya kazi. Kwa miaka 20, amekuwa shabiki wa dhati wa Bayern FC kwa mtazamo maalum: Naupenda mchezo, wakati mwengine ni kama sanaa, lakini wakati mwengine hua niko karibu sana na mchezo wenyewe kwa hiyo hujisogeza kando kidogo kwa kuwa sitaki kutegemea kitu ambacho siwezi kukidhibiti."
Andy Brassell (London, England) - Mwandishi wa habari wa michezo
Andy ni mwandishi wa habari wa gazeti la "The Guardian" na ni mtaalam katika kituo kiitwacho "Talksport". Maoni yake yana uzani na mada anazozingumzia hasa ni uhusiano baina ya vilabu vya Uingereza na Ujerumani. "Wachezaji wa Bayern Munich ni wakubwa na waliopata ufanisi wa kiasi kikubwa kiasi ya kwamba watu wengi hapa Ujerumani wanaona soka ya Ujerumani na ile ya Bavaria ni sawa tu."
Jaime Rodríguez Carrasco (Madrid, Spain) - Mwandishi wa habari wa michezo
Mwandishi wa habari huyu mwenye umri wa miaka 38 na anayefanya kazi katika gazeti la "EL MUNDO" anapenda mpira - kama kitu cha kujiburudisha na kama mashindano ya michezo. "Nikiwa Madrid naweza kujua kama mji huo una utulivu au hauko katika hali nzuri." Kwake yeye mechi bora ya msimu nchini Uhispania sio "El Clasico" bali ni pale Real Madrid wanapocheza na Bayern Munich.