Kutekwa nyara kwa wahudumu wa Medicins Sans Frontiers nchini Kenya
14 Oktoba 2011Matangazo
Wahudumu hao walikamatwa karibu na kazi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko kaskazini mwa Kenya. Pindi baada ya tukio hilo, polisi walianzisha operesheni maalum ya kuwasaka wahalifu hao kwa ndege na magari. Duru zinaeleza kuwa usalama umeimarishwa katika eneo hilo na mpaka wa Kenya na Somalia umefungwa kwa sasa. Jee, tukio hilo lina athari gani kwa Kenya? Hilo ndilo suali Thelma Mwadzaya alilomuuliza Simiyu Werunga, mchambuzi wa masuala ya usalama wa Kenya.
Mwandishi: Thelma Mwadzaya
Mhariri: Saumu Mwasimba