1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutana na Dk. Hawa Abdi: Mwanamke wa shoka Somalia

10 Juni 2011

Huyu ni mwanzilishi wa Wakfu wa Dokta Hawa Abdi na mwanamke wa kwanza nchini Somalia kufanyakazi na kumiliki hospitali binafsi katika nchi hiyo iliyosambaratishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo miwili sasa.

https://p.dw.com/p/11YMW
Wakimbizi wa Kisomali
Wakimbizi wa KisomaliPicha: Bettina Rühl

Mara baada ya kumaliza masomo yake ya udaktari, katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, Dokta Hawa Abdi alirudi Somalia na mwaka 1983 alifungua zahanati yake binafsi kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wanawake na watoto. Ni mmoja ya wanawake wa kwanza nchini Somalia kuwa madaktari wanaotibu magonjwa ya wanawake.

Halima Nyanza anaangalia maisha na kazi za mwanamke huyu wa aina yake.