You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: PantherMedia/picture alliance
Picha: PantherMedia/picture alliance
Kurunzi Afya
DW Kisuaheli inakuletea vidio maalumu kuhusu masuala ya afya.
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Unajua namna Yoga inavyoweza kukusaidia kiafya?
Nina uhakika unajua kitu kuhusu mazoezi ya Yoga, lakini unajua umuhimu wake kiafya? Kuna mengi unayoweza kujifunza ama kumshirikisha mwenzako kuhusu mazoezi haya. Tizama video hii kujifunza zaidi. #Kurunzi
Dalili za tatizo la PCOS kwa wanawake
Wanawake wengi wenye ndevu ama nywele za usoni wanakabiliwa na matatizo ya kiafya ya PCOS yanayohusiana na homoni. Dalili nyingine za PCOS ni kuongezeka uzito, uso wenye mafuta na ugumu wa kubeba ujauzito. #kurunziafya #wanawake #pcos #afya
Fahamu namna ambavyo mionzi dawa inavyotengenezwa Tanzania
Cyclotron Kiube ni aina Mionzi dawa ambayo hutumika katika uchunguzi wa awali wa saratani kwa kupiga picha kwa kutumia PET-CT Scan ili kujua hatua ya saratani na kumsadia mtaalamu kujua ni aina gani ya dawa ambayo itakua na msaada kwa mgonjwa.
Matumizi yaliokithiri ya muguka na madhara yake kiafya
Matumizi mabaya ya muguka na dawa zingine za kulevya yamesababisha ongezeko kubwa la waraibu katika vituo vya kurekebishia tabia. Hata hivyo viongozi wa Mombasa kupiga marufuku usafirishwaji na uuzwaji wa aina hiyo ya bidhaa. Tazama video kuona madhara yake kiafya.
Mafuriko yaacha homa ya mapafu kwa watoto Kenya
Mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko zimeacha athari za kiafya kwa watoto wengi katika maeneo ya mabanda nchini Kenya
Kutibu majeraha yaliosababishwa na vita Ukraine
Zaidi ya wanajeshi elfu ishirini waliojeruhiwa walifika katika hospitali ya Mechnikov katika eneo la Dnipro, tangu Urusi ilipoivamilia kikamilifu Ukraine mnamo Februari 2022. Daktari Valentyna Lisnycha katika hospitali hiyo inayotibu wanajeshi waliojeruhiwa vitani pamoja na timu yake wamejitolea kuokoa maisha ya askari.
Unalifahamu vipi tatizo la Usonji?
Ugonjwa wa Usonji au Autism ni tatizo la kibaiolojia ambalo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, huathiri mtoto mmoja kati ya kila watoto 100 duniani. Dalili zake huanza kuonekana mapema sana, kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Ni vigumu kugundua dalili zake. Lakini kwenye video hii unaweza kujifunza mengi.
Joto kali lina athari gani mwilini ?
Daktari Jalab Ashraf atowa maelezo zaidi jinsi ya kuhakikisha tunabakia imara kiafya katika kipindi hiki cha joto kali.
Hisia za kutojiamini
Umewahi kupata hisia za kutojiamini? Wanasaikolojia wanasema hisia hizo huchangiwa na mambo tofauti ikiwemo malezi na tabia binafsi. #Kurunziafya inatizama hisia hizo, ambazo si ugonjwa lakini hutupata katika maisha yetu ya kila siku.
Mpango wa kukopa na kulipia deni la matibabu Nigeria
Kutana na kikundi cha kijamii kutoka katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria, ambacho kinasaidia kaya masikini kulipa madeni ya matibabu hasa kwenye maduka ya dawa, lakini hata hivyo mpango hausadii tu watu masikini pia unaziwezesha biashara za dawa kustawi.
Ulaji wa chakula usiofaa chanzo cha matatizo ya afya
Profesa Janabi wa Muhimbili Tanzania anasema watu hawajakatazwa kula ispokuwa wale kwa mpangilio ili kutunza afya.
Teknolojia ya kuodoa uvimbe mwilini bila upasuaji
Utaalamu huu unaweza kutolewa kwa watu waliona uvimbe katika sehemu mbalimbali za mwili
Hamasa ya wahudumu katika vyumba vya kuhifadhi maiti
Wengi wamekuwa na mawazo tofauti juu ya watu wanaotoa huduma katika vyumba vya kujifadhi maiti katika hospitali na utakubali kwamba kumekuwa na hadithi nyingi kuwahusu na wakati mwingine hata zikitia hofu, lakini hebu tazama video usikie hadithi zao wenyewe wakisimulia juu ya hamasa inayowafanya kuipenda kazi yao adhim.
Tiba ya jino ya Root Canal
Ni lini mara ya mwisho uliumwa jino? Yale maumivu kiasi cha kuona giza wakati ni mchana😆😆😆 Je huwa una utaratibu wa kwenda kwa daktari wa meno kabla hujakumbwa na zahma kama hii? Na je, ulitibiwaje? Hebu msikie kijana huyu ambaye siku moja alikwenda bila ya kusukumwa hospitalini baada ya kuumwa jino na usikie alitibiwaje? Itakusaidia. #kurunziafya
Tatizo lenye kusumbua mfumo wa uzazi
Si kila shida ya mfumo wa uzazi, inaweza kuwa ugumba. Itazame vyema vidio hii ya Fathiya Omar labda, wewe, ndugu zako na wale wanaokuzunguka wanaweza kupata ufumbuzi katika kutafuta mtoto.
Lifahamu tatizo la Anorexia Nervosa
Kwa lugha nyepesi, Anorexia Nervosa ni hali ya kiafya inayomfanya mtu kuogopa kuongeza kilo au kuwa mnene.
Uboreshaji wa mpangilio wa meno kinywani
Kuwa na meno yaliyopangika vizuri huweza kukuongezea ujasiri unapozungumza na pia kufanya tabasamu lako liwe la kuvutia. Kinyume chake ni kwamba unaweza kupoteza ujasiri unapozungumza, unapotabasamu au unapocheka. Je unawezaje kuboresha mpangilio wa meno yako? Tazama vidio hii ya Kurunzi Afya.
Silke: Nimepewa moyo na mapafu kutoka kwa mfadhili nisiemjua
Maisha ya Silke Schulze yamenusurika baada ya kupata moyo na mapafu kutoka kwa mchangiaji alieidhinisha kuondolewa viungo vyake punde tu baada ya kufariki, mfumo huo umesaidia watu wengi waliokuwa wanahitaji msaada, sasa anaishi kwa kushuru kwa hisani isio mithilika.
Wakaazi Abidjan waweka mifumo ya maji taka kulinda afya
Taka imekuwa ni kero kubwa na kuhatarisha afya ya jamii katika moja ya kitongoji katika mji wa kiuchumi Ivory Coast Abidjan, kundi la vijana limeamua kutosubiri mamlaka kuchukua hatua, wameamua kutengeneza mifumo ya maji taka ili kuondoa tatizo kadhalika kuleta ustawi wa afya ya jamii katika eneo husika.
Fahamu jinsi maji ya ´dripu´ yanavyotumika kama tiba
Fahamu jinsi maji ya ´dripu´ yanavyotumika kama tiba
Kisukari chaleta hatari kwa Watanzania
Licha ya hatari ya ugonjwa huu, nusu ya watu walio na ugonjwa wa kisukari hawajui.
Mchakato wa utungishaji mimba kwa wanawake- IVF
Watu wanaokabiliwa na tatizo la kupata ujauzito baadhi hutumia njia ya maabara ya kupandikiza mimba, katika video ya Kurunzi afya leo tunaangalia mchakato huu namna ulivyowanufaisha baadhi ya wanawake kadhalika changamoto zake kwa watumiaji.
Maisha ya watoto wenye ugonjwa wa Hydrocephalus
Watoto wenye tatizo la kuvimba kichwa wanaweza kutibika na kuishi katika maisha ya kawaida. Zaidi Tazama vidio iliyondaliwa na Ibrahim Swaibu akiwa Kampala.#kurunziafya
Afya Yako: Maambukizo ya Ukimwi kwa vijana wadogo Kenya
Idadi ya maambukizo ya Ukimwi kwa vijana walio na umri mdogo nchini Kenya yako juu.
Mlipuko wa virusi vya Rota mjini Mombasa
Jiji la Mombasa nchini Kenya limekumbwa na ,lipuko wa Rotavirus, ugonjwa unaosababisha kutapika na kuharisha miongoni mwa watoto. Je, Rotavirus inatokana na nini na nini tiba yake?
Roboti "Da Vinci" lapandikiza mapafu kwa binadamu.
Kwa mara ya kwanza, hospitali moja nchini Uhispania imeweza kupandikiza mapafu ya binadamu kwa kutumia mbinu ya upasuaji wa roboti aliyepewa jina la "Da Vinci". #kurunziafya
Madhara ya kuvaa viatu virefu
Unafahamu kuwa viatu virefu vina madhara kiafya? Kufahamu zaidi fuatana nasi hapa umsikie mtaalamu akifafanua zaidi katika video hii ya Kurunzi ya Afya.
Fahamu dalili za awali za mtoto mwenye maradhi ya moyo
Takwimu mbali mbali zikiwemo za Shirika la Afya Ulimwenguni ,WHO, zinaonesha kuwa watoto wengi hufariki kabla ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo bila kugundulika na kupatiwa matibabu ya haraka. Kurunzi afya inaangazia dadili za awali za ugonjwa huo kwa watoto.#Kurunzi Afya
Kifua kikuu chawatesa wanaume kuliko wanawake nchini Kenya-Ripoti
Ripoti ya utafiti mpya uliofanyika nchini Kenya, imeonyesha kuwa theluthi mbili ya watu wanaougua kifua kikuu (TB) nchini humo ni wanaume. Sababu mojawapo ya hali hiyo, ni kuwa wanaume hupenda kujumuika kuliko makundi mengine katika jamii. Serikali ya nchi hiyo imeelekeza juhudi katika kuwakinga wanaume na ugonjwa huo na mengine kadhaa yanayowaandama.#Kurunzi Afya
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 1
Ukurasa unaofuatia