Kura ya maoni Venezuela
2 Desemba 2007Matangazo
Caracas:
Wananchi wa Venezuela wanaamua katika kura ya maoni leo kuhusu mpango wa marekebisho ya katiba yaliopendekezwa na rais Hugo Chavez pamoja na bunge la nchi hiyo. Zaidi ya wanajeshi 100,000 wako mitaani katika mji mkuu Caracas na miji mengine, kuhakikisha usalama. Miongoni mwa mambo mengine, mabadiliko hayo yataondoa kikomo cha kugombea urais na kusitisha uhuru wa Benki kuu ya Venezuela. Rais Chaves anasema mabadiliko hayo yataupa umma madaraka zaidi.
Wapinzani wake wamemshutumu kuwa anajaribu kun´gan´gania kubakia madarakani na wamewataka wapiga kura kuisusia kura hiyo ya maoni.