1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni Uingereza

Halima Nyanza6 Mei 2011

Wapiga kura nchini Uingereza wamekiadhibu chama cha Kiliberali nchini humo kwa jukumu lake lake la kupunguza nakisi serikalini, na kukitelekeza katika kura ya maoni iliyopigwa jana.

https://p.dw.com/p/11AfR
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron (kulia) na msaidizi wake, Nick CleggPicha: picture-alliance/dpa

Matokeo ya awali ya kura ya maoni iliyopigwa jana nchini Uingereza yanaonesha kuwa wafuasi wa chama cha cha kiliberali wametoswa na kuungwa mkono wahafidhina walio wengi.

Akizungumza matokeo hayo ya uchaguzi Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza kutoka chama Kiliberali Nick Clegg amekiri kuwa chama chao kimepata pigo katika uchaguzi huo wa jana na kuongeza kusema kuwa watahitaji kujifunza kutokana na yaliyowakuta.

Amefafanua pia kwamba katika maeneo ya nchi ambako walikuwa na wasiwasi kuhusiana na mipango hiyo ya kupunguza nakisi ambayo wanatakiwa kuiweka, ni wazi kuwa wanapaswa kulaumiwa.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na afisa wa ngazi za juu katika chama cha kiliberali Danny Alexander amesema vyama vilivyo serikalini, vinapoamua kuchukua uamuzi mgumu, husumbuliwa sana wakati wa chaguzi.

Umaarufu wa chama hicho cha kiliberali umeshuka tangu kuingia serikalini na wahafidhina mwaka uliopita na kufanya serikali ya kwanza ya muungano ya Uingereza tangu vita vikuu vya pili vya dunia.

Hali hiyo inatoa changamoto pia kwa kiongozi wa chama hicho cha kiliberali Nick Clegg, lakini hata hivyo afisa mwingine mwandamizi wa chama hicho, Waziri wa Nishati Chris Huhne amesema sasa sio wakati wa kutafuta kiongozi mpya. 

Kutokana na matokeo hayo mabaya waliyopata Waliberali kimewafanya wachambuzi wa masuala ya siasa kujiuliza iwapo serikali ya muungano itasambaratika na kuchelewesha hatua hizo kali zinazotaka kuchukuliwa.

Lakini hata hivyo mawaziri kutoka pande zote, Waliberali na Wahafidhina waliupuuzia mtazamo huo.

Matokeo rasmi ya mwisho yanatarajiwa kutolewa hii leo jioni.

Hatua hiyo juu ya mageuzi ya sheria za uchaguzi, iwapo nchi hiyo inabidi kufuata mfumo mpya wa kuchagua wabunge au la, ilizua mjadala mkali katika serikali ya muungano ya Uingereza.

Mwandishi: Halima Nyanza(reuters)

Mhariri:Josephat Charo