Kupigwa marufuku adhabu ya kutumia viboko kwa watoto mashuleni nchini Kenya
24 Julai 2008Matangazo
Mashirika hayo yamesisitiza kwamba serikali mpya ya nchi hiyo itabidi kuchukua hatua dhabiti katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa nchini humo.Itakumbukwa kwamba mwaka 2001 Kenya ilipiga marufuku adhabu ya kutumia viboko shuleni dhidi ya wanafunzi lakini marufuku hiyo haitekelezwi kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mashirika hayo mwaka jana.
Saumu Mwasimba alizungumza na Gilbert Onyango mmoja wa viongozi katika Muungano wa mashirika ya kutetea haki za watoto nchini humo CRADLE ambaye kwanza anafafanua zaidi ya mapendekezo yao kwa serikali ya Kenya kuhusiana na suala hilo.