Kundi la wanaharakati Zanzibar ladai kura ya Maoni kuhusu Muungano
11 Aprili 2012Matangazo
Huko Zanzibar Tanzania, kundi la watu walikusanyika leo (11.04.2012) katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuitishwa kura ya maoni kuhusu suala la Muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar 1964 na kuundwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliopo hii leo.
Mohamed Abdul-rahman alizungumza na Rashid Hadi anayedaiwa kuwa kiongozi wa kikundi hicho na kwanza anaelezea sababu za kukusanyika kwao.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Daniel Gakuba